Google PlusRSS FeedEmail

IRENE UWOYA APIGWA MKWARA MZITO

MUIGIZAJI wa filamu wa bongo movi, Irene Uwoya, ajikuta katika wakati mgumu baada ya kupigwa mkwara mzito na mwanamke anayedaiwa kuibiwa mpenzi wake na mwanadada huyo.

Hivi karibuni baadhi ya magazeti pendwa yalimripoti mwanadada huyo kujihusisha na mahusiano mapya ya msanii wa bongo fleva ambaye pia ni mwalimu wa kucheza muziki kutoka THT anayejulikana kwa jina la Msamii.

Ambapo kwa mujibu wa mahojiiano kupitia kipindi cha Clouds redio, mwanadada huyo Rehema, ambaye inasemekana alikuwa na mahusiano na mwanaume huyo kabla 'hajazama' kwenye penzi motomoto kwa msanii huyo wa bongo movi Uwoya.

Alisema kuwa anamshanga muigizaji huyo kwa kitendo alichokifanya ambacho kinamdharilisha kwani anajishushia heshima kwa jamii."Mimi namshangaa huyo mwanadada, Uwoya ndio maana anashindwa kuheshimiwa na tangu mahusiano yao yalivyoanza nilikuwa naambiwa lakini mwanaume wangu hawezi kuniacha mimi najua hizo ni tamaa za pese" alisema Rehema.

Inadaiwa kuwa msanii huyo Uwoya ametumia fedha kumshawishi mvulana huyo kukubali kuwa naye, ambapo Rehema alidai kuwa mwanaume huyo alimwambia Uwoya kuwa anahuhusiana na mwanamke mwingine na akakubali kuwa naye kwenye uhusiano mpya.

Kwa kupitia mahojiano hayo ya Clouds redio, mwanadada huyo aliweka wazi kuwa hamuogopi msanii huyo kwa kitendo alichokifanya kwani anajidharilisha mwenyewe.


This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging