Google PlusRSS FeedEmail

P-FUNK ATEMBELEA KABURI LA NGWAIR

MTAYARISHAJI wa muziki wa kizazi kipya nchini P-Funk Majani, ameongoza msafara wa watu mbalimbali mashuhuri wakiwemo baadhi ya wasanii wa muziki, kutembelea kaburi la msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini Albert Mangwair 'Ngwair'.

Ziara hiyo ilifanyika jana  ikiwa ni moja ya maadhimisho ya kutimiza mwaka mmoja tangu kifo cha msanii huyo kilipotokea ambapo P-Funk na wenzake walitembelea kaburi hilo lililopo mjini Morogoro.

Ambapo wasanii hao walipata fursa ya kusali kwenye kaburi hilo na kuwasha mishuaa ikiwa ni moja ya kumuenzi msanii huyo.

Akizungumza na blog hii kwa njia ya simu, P-Funk alisema kuwa kutembelea kaburi hilo ni kuonesha kwa jinsi gani wanavyomkumbuka kwa vitendo,kwani kwao alikuwa ni zaidi ya rafiki.

May 28 mwaka jana ndio siku iliyotangazwa msanii huyo kufariki dunia akiwa yupo nchini Afrika Kusini, inakodaiwa kuwa alikwenda kwa ajili ya shughuri ya kimuziki.

Alipatwa na umauti jijini Johannesburg, Afrika Kusini katika hospitali ya St. Helen...May 28, mwaka jana na kuacha pengo kubwa lisilozibika katika sanaa ya muziki wa kizazi kipya. Apumzike kwa Amani.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging