Google PlusRSS FeedEmail

BARAFU ALIA NA FUJO ZA AFRIKA KUSINI

Msanii wa bongo movie Suleiman Said Barafu amesikitishwa na vitendo vya baadhi ya raia wa afrika kusini kuwafanyia fujo raia wakigeni waliomo ndani ya nchi hiyo.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Barafu alisema “Sio tu msanii wa bongo movie bali kila mwanadamu hatafurahishwa na vitendo vile vilivyotokea huko Afrika Kusini”. Barafu alienda mbali zaidi na kuwaita raia hao sawa na Makaburu.

“Tunakumbuka vitendo kama hivi vilikua vinafanywa na Makaburu kwa raia wa Afrika ya Kusini, lakini eti leo hii vinafanywa na Waafrika KIusini, tena kwa Waafrika wenzao?” aliuliza Barafu.

Akizungumzia upande wa bongo movie, Barafu amekanusha taarifa zinazozagaa mtaani kwamba bongo movie siku hizi haina mvuto baada ya kufariki Kanumba.
Sio kweli kwamba bongo movie imekufa na haina mvuto bali hayo ni maneno tu ya watu. Kuhusu kufanya kazi kimataifa mbona Mlela na Cloud wamefanya kazi nchini Uingereza na bado wengine wamepata tuzo marekani msanii kama Omari na Tiko” alieleza Barafu. Barafu ametumia nafasi hiyo kuwataka mashabiki wasubiri kazi nzuri na yenye ubora, ya filamu yake itakayotoka hivi karibuni aliyomshirikisha Hashimu Kambi, Patcho Mwamba na Irene Poul.Pia amelitaja jina la filamu hiyo kuwa itaitwa Masumbuko na imefanyaka chini ya kamapuni ya Leo Media

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging