Google PlusRSS FeedEmail

BEN POUL HAYUKO TEYARI KUPIGA KURA

Mkali wa RNB anaeiwakilisha Dodoma, Bernard Paul “Ben Poul” amedai yupo tayari kuipigia kura katiba inayopendekezwa ikiwa tu Maslahi ya wasanii yatahusishwa kwenye katiba hiyo.

Ben aliyazungumza hayo alipozungumza na Azam TV, mapema leo asubuhi akidai yeye si mfuatiliaji mzuri wa masuala ya kisiasa ila linapokuja kwenye maslahi ya kazi yake ni muhimu kuhusika kwenye harakati hizo.

“Mimi unajua sifatilii sana siasa, ila kuhusu katiba itabidi niseme jambo coz mimi kazi yangu inabidi iwemo mule, nitaangalia kwanza maslahi yangu mule kama yapo basi nitapiga kura, unajua ifike mahali hata mameneja wapate pesa ya kutosha kupitia huu huu mziki yani” alisema Ben poul

Pia alikiri hivi sasa ana menejimenti ambayo inamsimamia vizuri katika mziki, huku akiwataja Vanessa Mdee na Nah Reel kuwa chini ya menejimenti hiyo.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging