Google PlusRSS FeedEmail

HUSSEIN MACHOZI AKANUSHA TAARIFA ZA KIFOMwimbaji  Hussein Machozi ameshtumu uvumi unaondelea kwamba amefariki baada ya ajali mbaya ya barabarani iliotokea katika mji wa Dodoma nchini Tanzania siku ya jumatano.

Habari za kifo chake zilianza kuenea katika mitandao ya kijamii baada ya ajali hiyo ambapo mtu mmoja aliyeonekana kufanana na msanii huyo alifariki kutokana na majeraha.
Hussein amesema kuwa yuko hai na buheri wa afya kupitia mtandao wake wa facebook ambapo alisema kuwa habari hizo zilimwacha mamaake na dadaake wagonjwa baada ya kuzirai waliposikia habari hizo.

Huu ndio ujumbe alioandika katika mtandao wake wa facebook.

{Nilijiandaa hapa nimekwenda mazoezini kucheza mpira, niliacha simu yangu kwenye charge na niliporudi baada ya mazoezi nakuta missed calls nyingi sana, msg na simu za mama yangu pamoja na dada, wakati najiandaa kuanza kupiga simu ghafla naanza kupata simu za watu mbalimbali kwamba nimepata ajali na kufariki, mimi nikawaambia sio kweli mimi ni mzima na nipo}

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging