Google PlusRSS FeedEmail

JONI MITCHELL ALAZWA ICU

Mwanamuziki na mtunzi wa nyimbo nchini Marekani Joni Mitchell amelazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi baada ya kukutwa akiwa amepoteza fahamu nyumbani kwake Jijini Los Angeles.

Mitchell alikimbizwa hospitali jana mchana saa za Marekani, na taarifa iliyotolewa kwenye tovuti yake imesema msanii huyo alirejewa na fahamu akiwa ndani ya gari la wagonjwa akielekea hospitali.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa mshindi huyo wa tuzo nane za Grammy, kwa sasa amelazwa kwenye chumba cha wagonjwa mahututi akipatiwa matibabu na hali yake inaimarika.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging