Google PlusRSS FeedEmail

LINEX: "KILA MSICHANA NINAYEACHANA NAYE TUNAKUA MAADUI"

                   
                              
Hit maker wa Salma Sunday Mjeda “Linex” amefunguka ya moyoni na kudai kuwa katika mahusiano yake ya kimapenzi, hakuwahi kuachana na mwanamke yeyote bila kuwa maadui.

Linex anapasukia kuwa anashangaa mambo kuwa tofauti kwa mpenzi wake wazamani, dodo (mzungu) kwani wameachana kitambo kirefu lakini still bado ni marafiki na wanashauriana mambo mbalimbali ya kimaisha. Kupitia ukurasa wake wa facebook Linenga ameshare uzoefu wake katika hilo.

“Jaman eeeeeeh this is my fb acount kila mtu hua anaandika anachojiskia post yangu ya mwisho kwa siku ya leo naomba na mm niongee nachojiskia ki ukweli toka nimejua Kumpenda mtoto wa kike au kua kwenye mahusiano sijawahi kuachana na mtu alafu mahusiano yanapokwisha yule mtu asiwe adui yangu lakini kwa binti huyu imekua tofauti sana hatuko pamoja lakini tumebaki kua marafiki wazuri tunashauliana tunajaliana tuna heshimiana na kila mtu kati yetu ana support kazi ya mwenzake sikujua uzuri wa kumfanya mpenzi wako wa zaman awe rafiki yako wa karibu Je una urafiki na mpenzi wako wa zamani? au mmekua maadui? aka paka na mbwa? Nachomaanisha ni kwa kua hatukuzaliwa pamoja na leo hatuko pamoja basi staki kua na uadui na wadada ambao nishawahi kua na mahusiano nao tuwe marafiki basi Dear Ex usinichukie nisikuchukie haikupangwa thats why hatuko wote Nisaidie kumtag ex wako na mwambie tuwe marafiki kama una uadui nae haijalishi nini chanzo cha kutengana mbarikiwe sana.” Aliandika Mjeda

Ni mwaka mmoja umekatika tangu Linex aachane na mtasha huyo.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging