Google PlusRSS FeedEmail

MAJUNGU TENA TIP TOP CONNECTION?

Moja kati ya wasanii wakali wanaounda familia ya TipTop connection manzese, Khaleed “Tunda man” amefunguka mambo kadhaa kuihusu crew hiyo.

Kupitia “The jump off” ya Times FM na Jabir Saleh, mkali huyo wa msambinungwa amekiri Tip top ya miaka ya nyuma ilikuwa vizuri zaidi isiyo na majungu ukilinganisha na ya sasa.

“Nakubaliana na wewe Tip Top ya enzi zile za tunapanda ilikuwa kama timu ya taifa vile, maana umoja ulikuwepo na wala hakukuwa na majungu yani kila mmoja alisimamia nafasi yake” alisema Tunda

Kwenye line nyingine alisanuka kuwa, katika watu ambao anatamani warudi tena kundini humo ni mkali kutoka maza bay Tanga Cassim Mganga.

“Kiukweli Cassim natamani arudi yani kwakuwa, bado hatujampata mbadala wake,unajua sauti yangu na yake(Cassim) zilikuwa zinaendana sana na Madee akipita na bass basi inakuwa poa sana, kwa kweli hakuna aliyeziba pengo lake” alimaliza

Tunda ameenda mbali zaidi kwa kusema baada ya kuondoka kwa Cassim Mganga, Tip top imeyumba.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging