Google PlusRSS FeedEmail

MCHEPUKO YA WARIDI IKO NJIANI

            Mchepuko Film

MWIGIZAJI mkongwe katika tasnia ya filamu Anna Constantino ‘Waridi’ anashuka na mzigo mkali wa filamu mpya ya Mchepuko iliyoshehena mastaa kibao kwa ajili ya kutoa burudani kwa wapenzi wa filamu Bongo filamu hiyo inasambazwa na Proin Promotions ya Jijini Dar.

Mmoja kati ya wasanii washiriki wa filamu hiyo Kulwa Kikumba ‘Dude’ amedai kuwa sinema yao inaonyesha uwezo wa wakongwe katika tasnia ya filamu Swahilihood huku akijivunia aina ya uigizaji wa Waridi pamoja na wasanii wengine walioshiriki kutengeneza sinema ya Mchepuko.

“Msanii kama Waridi ni mwigizaji mwenye uwezo mkubwa na mwasisi wa fani ya uigizaji Bongo kwani kumbuka hawa ndio wasanii waliofungua njia kwa sisi sote ambao ndio tunaigiza filamu na tamthilia,”anasema Dude.

Filamu ya Mchepuko inawashirikisha wasanii kama Cathy Rupia, Dennis Sweya ‘Dino’, Waridi mwenyewe Kulwa Kikumba ‘Dude’ na wasanii wengine nyota kibao wanaofanya vizuri katika tasnia ya filamu.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging