Google PlusRSS FeedEmail

MIAKA 3 MARA BAADA YA KIFO CHA KANUMBAIlikuwa siku ya tarehe 7 mwezi April 2012 pale nyota iliyong’ara katika tasnia ya filamuTanzania ilipozima ghafla, alikuwa ni msanii muongozaji na mtayarishaji wa filamu Steven Charles Kanumba ‘Kanumba’ awali ilikuwa kila inapofika tarehe kama hiyo na mwezi huu kuna tukio kubwa lilitokea kwa ajili ya kumbukumbu yake.

Lakini kwa mwaka huu hilo halikufanyika zaidi ya mama mzazi wa msanii huyo Frola Mtegoa kwenda baadhi ya wasanii wachache wanaoshuhudia pengo lake na kukosa kazi dio pekee walifika katika makaburi yaliyopo Kinondoni kwa ajili ya kukumbuka siku muhimu kwa msanii huyo aliyejijengea sifa kubwa Afrika Mashariki na kwingineko.

Uchunguzi uliofanywa  umebaini baadhi ya mambo makubwa yanayotokea baada ya kifo cha Kanumba, moja ambalo lina athari kubwa ni wale wasanii wote walikuwa wakifanya kazi na marehemu kutengwa na watayarishaji wengine kwa kutoshirikishwa filamu nyingine kulingana na kazi walizokuwa wakifanya awali.

Ni miaka mitatu watu walikuokuwa wanafanya kazi na kampuni ya Kanumba The great Film hawana kazi kutoka kampuni yoyote hata kushindwa kuendelea kuwepo katika ofisi aliyoiacha marehemu kutokana na gharama za pango, hata kuzalisha filamu za kampuni haiwezekani tena, hali si shwari.

Tunaongea na meneja wa kampuni hiyo Novatus Mayenja ‘Nova’ anasema kuwa toka kifo cha bosi wake hali imebadilika na kuwa mbaya kwani hata wale watayarishaji waliokuwa wakiwahitaji hawawapi tena kazi na haelewi kuna uoga gani hadi itokee hali hiyo.

“Kwetu kila inapofika siku ya kumbukumbu ya Kanumba inatuuma sana kwani karibia wote tuliokuwa katika kampuni yake tumepoteza ajira, hatuna ajira za uhakika kama alipokuwepo yeye hakuna mtu alikuwa mnyonge,”anasema Nova.

“Angalia mimi Zakayo Magulu, Mayasa Mrisho ‘Maya’ Kiuno, Steve hatuna ajira njaa itatuua, naongelea hapa njaa ya sanaa siyo ya tumbo, sasa ndio rahisi kugundua rafiki wa kweli si hauna kazi utakayolipwa pesa nyingi,”anasema Nova.

Ni kweli hata wasanii waliotolewa na Kanumba hasa watoto wadogo kama Hanifa Daud ‘Jennifer’, Patrick na wengineo hadi sasa watayarishaji hawajawatumia kabisa katika filamu zao na kuwaacha vipaji vyao vikifa, ni wazi hakuna kitu cha kumuenzi Kanumba pamoja kulitangaza Taifa kimataifa.

Hali ya soko

Hali ya soko ni mbaya kwani toka kifo cha Kanumba soko limetikisika kumbuka msanii huyo alipofariki ghafla filamu zote alizocheza ziliuzwa sana pasipo kuchagua kama za zamani, siku ya mazishi yake ni siku iliyokuwa ya neema kwa wengi kwa kila kitu kilichomhusisha Kanumba kiliuzika fulana, vitabu nk.
                 

                                                                  Kanumba akiwa na Rose Ndauka

Baada ya soko kuwa baya hivi karibuni kampuni aliyokuwa akifanyanayo kazi ya usambazaji ilinunua filamu kutoka Mbeya ambayo marehemu aliwahi kucheza na kuibadilisha jina kutoka Lethal Poison na kuiita Yamenikuta na kuingiza sokoni na kufanya vizuri jambo hili linafanya tukubaliane na imani za wale wanaoamini kuwa baada ya kifo chake soko limeyumba.

Kanumba ndio msanii pekee aliyekuwa akiangalia soko na kulinyanyua kwa kutafuta wasanii wanaofanya vizuri nje ya nchi, ameweza kushirikiana na wasanii kama Ramsey Noah, Mercy Johnson, Emmanuel France wasanii wakubwa kutoka Naijeria lakini toka kifo chake hakuna hata msanii aliyefanya juhudi hizo zaidi ya kurekodi sinema zetu Morogoro.

Kanumba alikuwa wa kipekee msanii huyu alifaririki tarehe 7.April. 2012 baada ya kudaiwa kusukumwa na msanii mwenzake Elizabeth Michael ‘Lulu’ sasa ni miaka mitatu toka kifo chake soko limedorora na wasanii wengine kukosa ajira, hata Ray anasema kuwa kutokuwepo Kanumba amekosa mshindani.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging