Google PlusRSS FeedEmail

MUIGIZAJI WA FILAMU MARK WAHLBERG ATENGENEZA FILAMU TUKIO LA MLIPUKO WA BOMU

Muigizaji nyota wa filamu Mark Wahlberg mzaliwa wa Boston atatengeneza filamu inayohusu tukio la mlipuko wa bomu la mbio za Marathoni za Boston za mwaka 2013.

Filamu hiyo itakayojulikana kama Patriot's Day itahusisha uigizaji wa msako wa siku tano wa ndugu raia wa Chechnya Dzhokhar na Tamerlan Tsarnaev, waliohusika na tukio hilo lililouwa watu watatu na kujeruhi zaidi ya 260.

Filamu hiyo pia itaweka wazi tukio la kuzingirwa kwa mtuhumiwa Dzhokhar Tsarnaev, ambaye kwa sasa anaumri wa miaka 21, na kutolewa kwenye boti aliyekuwa amejificha huko Watertown. Kaka yake Tamerlan aliuwawa awali katika mapambano nia polisi.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging