Google PlusRSS FeedEmail

NDOA YA KIMILA IMENISHINDA KWA KIPIGO- SHAMSA

               
                             
MWANADADA nyota yake iliyong’ara katika filamu ya Chausiku Shamsa Ford amefunguka moja ya sababu iliyompelekea kutengana na mzazi mwezake ilikuwa ni kipigo kutoka kwa mzazi mwenzake huyo ambaye amezaa naye motto mmoja anayejulikana kwa jina la Telly baada ya kuishi naye kwa muda.

“Nimekuwa nikivumilia mengi na hofu yangu ilikuwa ni taswira iliyopo kuwa wasanii nyota hawadumu katika ndoa hata pale nilipokuwa naumia nilikaa kimya nikiamini mwenzangu anaweza kubadilika hakukuwa na mabadiliko,”anasema Shamsa.Msanii huyo aliolewa na ndoa ya kimila na Dickson ‘Dick’ huko Musoma na kuishi kama mke na mume na kubahatika kupata mtoto mmoja, ambaye amekuwa kiunganishi cha wanandoa hao ambao tayari wameshamwagana, msanii huyo amedai kuwa baada ya kuachana na mumewe alikaa kimya lakini Dick alianza kutuma katika mitandao ya kijamii ugomvi wao.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging