Google PlusRSS FeedEmail

NICK MINAJ AWAPA FUMBO MASHABIKI WAKE


Nchini Marekani rapa wa kike Nicki Minaj kwa kupitia akaunti yake ya twitter jana amepost picha ya mkono wake huku kidole kikiwa kimevalishwa pete ya uchumba, ikisindikizwa na maneno haya “I’ll post it later,” kwamba atatoa ufafanuzi hapo baadae.

Taarifa zimesambaa kua Nicki Minaj amevalishwa pete hiyo na mpenzi wake ambae pia ni rapa anaefahamika kwa jina la Meek Mill.

Kwa mujibu wa mtandao wa online.com chanzo cha habari kinasema pete hiyo ina thamani ya kiasi cha dola laki tano za kimarekani. Chanzo hicho kilifafanua zaidi pete hiyo ni ya dhahabu na kueleza Nicki na Meek Mill wanatarajia kufunga ndoa hivi karibuni. Ndoa hiyo huenda ikawa kweli kwani mwezi wa pili mwaka huu Nicki aliwahi kukiri kwamba anahamu ya mtoto, lakini hawezi kupata mtoto akiwa nje ya ndoa hivyo ni lazima aolewe

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging