Google PlusRSS FeedEmail

SNURA AINGIZWA TOWN

  

MWIGIZAJI wa kike na mwimbaji wa muziki wa Bongo Fleva Snura Mushi ‘Mama wa Majanga’ simu yake ya mkononi imetekwa na wajanja wa mjini kwa kuswap na simu anazopigiwa yeye kwenda kwa mtu mwingine ambaye hata hamjui wala hana mahusiano naye na hajui alitumia njia gani kuiteka hajui.

               

Snura na mitego ya ajabu.


Snura katika pozi.


“Hata sielewi mtu huyu kafanyeje hadi namba yangu kuitumia yeye, na mbaya zaidi ni pale ambapo kila anapobahatisha namba ya rafiki yangu huomba atumiwe pesa nahisi lengo lake kuu ilikuwa ni kujipatia pesa kwa njia ya utapeli na kujiita Snura,”anasema Snura.

Katika kuepuka hilo msanii huyo ameamua kuiachana namba hiyo na anapatikana katika namba mpya ambayo anawasiliana na jamaa zake pamoja na wateja wake wanaomhitaji katika show za muziki hivyo kwa wapenzi wake waliokumbwa na mikasa ya tapeli huyu anawapa pole na wakiombwa fedha na mtu huyo wasimtumie ni muongo.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging