Google PlusRSS FeedEmail

TAFF YAFANIKIWA KUWAPATANISHA JACK NA TICO

             Jackson Kabirigi, Timoth Conrad

BAADA ya kutengana kwa muda mrefu hatimaye leo hii magwiji wawili katika tasnia ya filamu Jackson Kabirigi ‘Jack’ na Timoth Conrad ‘Tico’ wamepatanishwa na Shrikisho la filamu Taff baada ya mazungumzo yaliyochukua saa kadhaa hadi kufikia muafaka na kurudi kama mwanzo iliyvyokuwa Timamu Effect.

Akiongea na wanahabari amesema kuwa amefurahishwa na kazi kubwa iliyofanywa na Rais wa Taff Simon Mwakifwamba kwa kutumia hekima zake na kumaliza tofauti iliyopelekea kujenga Uhasama wa kimanenoa kati ya wasanii hawa walioitangaza Tanzania kwa filamu yao ya Mdundiko.

“Moja ya kazi kubwa ambayo inabidi ifanywe na shirikisho ni kujenga umoja kwa wadau wake ambao ni wasanii pamoja na watayarishaji kwa ujumla wake, leo Tico na Jack kupatana na kurudi kufanya kazi pamoja tasnia itasonga mbele,”anasema Kallaghe.

Tico naye amesema kuwa anaamini kuhusu ushirikiano wao ambao unaweza kuleta tija katika utendaji wa kazi na anafahamu kuwa wanahitaji kuwa pamoja lakini sababu kubwa ni wapambe ambao walifanikiwa kuwafanya wawe mbali bila hata ya kujua ugomvi wao na kuiacha kampuni.

“Bongo Movie fitina ni nyingi sana msipokuwa imara mnageuka na kuwa maadui bila sababu ya msingi naamini kuhusu kolabo yangu na Jack nadhani naye ananihitaji kama ninavyomhitaji mimi sasa ni kazi hakuna maneno tena,”anasema Tico.

Kila mtu anajisikia faraja kuweza kutatua tatizo hili ambalo lilikuwa linaua tasnia ya filamu au kujenga pengo katika utendaji wa watu hawa wawili vijana wadogo wenye ndoto za kufanya kazi kimataifa na ubora wa juu, Jack mahiri katika uongozaji na Tico hatari sana katika utayarishaji effects...

“Nimefurahia kuwepo na ndugu yangu Tico tulikuwa na ndoto kubwa sana naamini ilikuwa kama likizo sasa tunarudi napenda kuwaahidi uongozi wa Taff na funs wetu kazi zile kutoka kwa Tico chini ya Director Jack zitashuka na kutikisa,”anasema Jack.

Naye Mwakifwamba amsema amefurahishwa sana na wasanii hao kuwa kitu kimoja kwani moja ya changamoto kuwa inayosumbua katika tasnia ya filamu ni hali ya wasanii na watendaji kujikuta wakiingia katika uhasama ambao haujengi bali kubomoa umoja ambao unahitaji sana.

“Mimi kama kiongozi si kiongozi wa kukaa ofisini tu bali ni kuhakikisha tunawajengea mahusiano mema na kutatua matatizo kwa wale tunaowaongoza, ni ushindi kwa Taff leo hii Jack na Tico wanapatanishwa na kuwa kitu kimoja,”anasema Mwakifwamba.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging