Google PlusRSS FeedEmail

UMOJA WETU KOMEDI UNAIMARIKA- SUMAKU


Mwenyekiti wa Chama cha Wachekeshaji (Tanzanian Comedian Association) Habib Mkamba ‘Sumaku’ amewapongeza wasanii hao kwa kujitolea katika kumuuguza msanii mwenzao hadi kifo chake Fadhil Said almaarufu kama Diffender, amedai kuwa pamoja na kutengwa na wasanii wengine lakini walijitoa.


“Nawashukru na kuwapongeza kwa wale wasanii wa Komedi ambao tumejitoa kupigania afya ya marehemu Difenda, niliwahi kusema kila anapofariki mwenzetu kuna mwingine yupo njiani tusiposhirikiana ni tatizo,”

“Komediani tumetengwa na wasanii wenzetu, sisi misiba yao tunashiriki lakini wao, hawapo naamini ushirikiano wetu imeimarika,”anasema Sumaku.

Mwenyekiti huyo aliyasema hayo baada ya mazishi ya msanii mwenzao aliyefariki siku ya jumamosi na kuzikwa na mamia ya watu na kuacha historia ya kipekee kwani Jeneza lake lilibebwa kutoka Kigogo Luhanga hadi Magomeni katika makaburi ya Mwinyimkuu.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging