Google PlusRSS FeedEmail

BASATA 'WATANZANIA HAWARIDHIKI' JUU YA TUZO ZA KILIMANJARO



Baraza la sanaa Tanzania (BASATA), limetoa tamko kuhusiana na malalamiko yanayotolewa mara kwa mara kuhusu tuzo mbalimbali dhidi yao.

Akizungumza kupitia kipindi cha “The jump off” cha Times fm, mratibu wa ufundi na maonyesho ya nje BASATA bwana Malegesi, amesema hua wanajitahidi kushughulikia malalamiko yanayoelekezwa kwao mara kwa mara na wamekuwa wakiyafanyia kazi kadri ya uwezo wao.

“Yani jinsi yanavyoletwa ndivyo tunavyo yashughulia, na tumekuwa tukifanya kwa weledi wa hali ya juu” alisema Malegesi.

Katika hali nyingine mratibu huyo ametolea ufafanuzi wa shutuma zinazoelekezwa kwao, kutoka kwa Watanzania na wasanii wakilalamikia upendeleo katika tuzo mbalimbali za muziki zinazofanyika nchini.

“Hakuna mtu yani sikiliza, tatizo kubwa la watanzania na wasanii hawaridhiki, hii ndio shida ya watanzania, shida yetu ipo kwenye kutambua kwamba kuna mtu anashinda na mtu anashindwa,hata kuingia kwenye kinyang’anyiro inapaswa uridhike” alimaliza Malegesi.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging