Google PlusRSS FeedEmail

CHRIS BROWN ATINGA KWENYE TUZO NA MTOTO WAKEMei 17 siku ya jumapili ilikua ni siku ya utoaji tuzo za chati ya Billboard ya nchini Marekani zilizofanyika kwenye jiji la Los Angel ambapo mastaa wengi nchini humo walihudhuria tukio hilo.

Kila staa alikua na aiana yake ya mtoko, lakini pengine Cris Brown alikua tofauti zaidi kwani aliamua kuingia katika ukumbi akiwa na mtoto wake Royalty ambaye mpaka sasa anaumri wa miezi 11.

Pamoja na kukosa tuzo lakini Chris Brown kuanzia mwanzo mpaka mwisho wa tukio alionekana mwenye furaha kuwa na mtoto wake siku hiyo, mtoto ambaye amezaa na mwana dada Nia Amey.

Wahudhuriaji wengi walimpongeza Chris kwa kuonyesha kumpenda binti yake, huku wengine wakihoji huenda Chris anamuandaa mtoto wake awe mwanamitindo kwa jinsi alivyomvalisha siku hiyo.

Bado haijajulikana ni upi utakua mufaka wa mapenzi kwa mwanamuziki huyo anaeongoza kwa kushirikshwa kwamba ataendelea kuwa na mapenzi ya kweli kwa mama wa mtoto wake Nia Amey, au ataendelea kuwa na mahusiano na mpenzi wake wa sasa Karrueche Tran.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging