Google PlusRSS FeedEmail

CHRISS BROWN AMTWANGA MWENZAKE NGUMI

Imeripotiwa siku ya jumatatu Chriss Brown akiwa na wenzanake ndani ya hotel ya Las Vegas alimpiga kijana mmoja ngumi wakati wakicheza mpira wa kikapu, na kwa bahati mbaya wawili hao walikumbana kimwili katika harakati za mchezo huo.

Polisi mmoja wa kituo cha Las Vegas wamesema Chriss Brown anaweza kusaini makubaliano ya kumaliza ugomvi huo au kama ikishindikana basi kesi hiyo itapelekwa mahakamani.

Bado jina la kijana huyo halijatambuliwa na baada ya tukio hilo kijana huyo alipelekwa hospital ya Sunrise kwa ajili ya matibabu kutokana na majeraha aliyoyapata.

Mpaka Chriss Brown hajatamka neno lolote juu ya sakata hilo, hivyo inasubiriwa ni nini atakachoamua.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging