Google PlusRSS FeedEmail

DIAMOND 'NILIONGA GARI NA NILIONEKANA SIFAHI'

HII ni kali zaidi msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini Ney wa mitego na Diamond Plutnums, wameamua kuzungumzia ukweli wa mahusiano yao kupitia nyimbo yao mpya inayojulikana kwa jina la Mapenzi au Pesa?.

Hii ishawahi kuzungumzwa na  mwanamuziki mkongwe aliyekuwa akiheshimiwa kwa misemo (quote) za kimaisha Mae West, aliwahi kusema kwamba ukitaka utambue hisia za mtu fuatilia aina ya muziki anaosikiliza na kama ni mwanamuziki sikiliza anachokiimba.

Ni hivi juzi tu Rapa Mabeste kazungumzia safari yake ya kimaisha na mkewe Lisa, na kaamua kuwakilisha hisia zake kupitia muziki, sasa Ney wa Mitego ametoa ngoma mpya aliyomshirikisha Diamond inaitwa “mapenzi au pesa” inayoonyesha ubishani wa mapenzi ya kizazi hiki, ni lazima uwe na mkwanja au mapenzi ya kweli?

Ukiisikiliza ngoma hiyo katika verse ya kwanza, ambayo kaimba Diamond amesema kama mapenzi ni pesa mbona yeye alitoa gari aina ya Toyota Murrano lakini akakimbiwa? Ina maana anakumbuka zawadi aliyoitoa kwa Wema Sepetu?

Kama unakumbuka vizuri Naseeb Abdul “Diamond”, aliwahi kutoa zawadi ya gari kwenye siku ya kuzaliwa ya aliyekuwa mpenzi wake muigizaji Wema Abraham Sepetu.

Wawili hao hawapo kwenye mahusiano hivi sasa, na moja kati ya sababu za kuachana ilielezwa kuwa baada ya Dangote kutoa gari hiyo mwanadada huyo ilidaiwa “Madame” alipokea gari ya thamani zaidi aina ya Benzi huku kukiwa hakuna maelezo ya kutosha ni wapi hasa limepatikana.

Katika line nyingine mmiliki wa hit “nitampata wapi”, amesikika akimpa makavu Ney kwenye wimbo huo kwa kumweleza “nasikia mbuzi kala mukeka binti kaenda kwao, mafundi wamemteka kakuachia mwanao” akimaanisha Siwema babes mama wa Ney.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging