Google PlusRSS FeedEmail

DIAMOND PLATNAMU AMUA KUFANYA KAZI NA ROPERROPEJuzi kupitia mtandao wa Instagram, kuliibuka mjadala mzito unaomuhusu “icon” wa Bongo flava kwa sasa Naseeb “Diamond” Abdul na desiner kutoka Los Angels Califonia Devontae Roper, ambaye nguo zake zimevaliwa na stars wakubwa duniani kama Chriss Brown, rapper Future pamoja na mkali wa RNB August Alsina.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Devontae ambaye brand yake inafahamika kama RoperRope aliweka picha ya Diamond akimshutumu vikali kwa kufoji shati yake(inayoonekana kwenye picha hapo juu),na kutumia brand yake bila ruhusa.

“I usually don’t blast people who make or wear fakes of my designs but this person went way too far when they used my logo! @diamondplutnumz is wearing fake #RoperRope shirt made by a person with bad character and strong lack or originality! This is not ok” aliandika Desiger huyo.

Kisanga hicho kilichogusa hisia za watu wengi, wengine wakimtetea Diamond kwamba yeye ni mnunuzi tu na lawama zote alistahili mshauri wake wakati wengine wakiungana na Rperrope kumtupia lawama Diamond kwa kuwa ni kinyume cha sheria.

Katika post nyingine aliyoiweka Designer huyo hapo jana, amekubali kufanya kazi na Diamond huku akizifuta post za nyuma alizokuwa akimshutumu Chibu.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging