Google PlusRSS FeedEmail

K LYNN AINGIA TASNIA YA MITINDOAliye kuwa miss Tanzania mwaka 2000,Jacquline Ntuyabaliwe maarufu kama “K Lynn” ambaye pia ni mwanamuziki wa Bongo Flava amefunguka na kudai kuwa hatamani na wala hafikirii kufanya tena muziki kwa sasa.

Akizungumza jijini Dar es Salaam,  Jack, amesema ni kitu ambacho alikifanya miaka mitano nyuma na sasa hivi ameshaacha kufanya muziki kwa kuwa kuna vitu vingine anafanya.

“Kuna vitu ambavyo unaweza kuzungumzia, its only news pale inapokuwa news ikishapita miaka mitano si news tena, na mi sitaki tena ku focus tena kuhusu muziki, kwa maana sifanyi tena hicho kitu na wala sikumbuki maisha yale ya kuimba tena” amesema Jacquline

Mlimbwende huyo ambaye pia ni mke wa mfanyabiashara maarufu nchini Reginard Mengi, amesema kwa sasa amegeukia tasnia ya mitindo(interior design) na si muda mrefu tutaanza kushuhudia kazi zake.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging