Google PlusRSS FeedEmail

KAMPUNI YA 50 CENT YAFIRISIKAKwa mujibu wa Patrick J. Neligan, Wakala na Mwanasheria wa kampuni ya kupromoti mchezo wa ngumi inayomilikiwa na Rapa pamoja na Mjasiriamali Curtis Jackson, a/k/a 50 ni kwamba kampuni hiyo imefilisika na inadaiwa madeni.

Kampuni hiyo inayotambulika kwa jina la SMS Promotions, ilianzishwa mwaka 2012 na tangu kipindi hicho imefanikiwa kupata umaarufu na kwa kuwasaidia baadhi ya mabondia ambapo mmoja wa mabondia hao ni bondia wa uzito wa kati James Kirkland.

Chini ya usimamizi wa 50 Cent kampuni hiyo ilionekana yenye jitihada za kufika mbali katika kuhakikisha inakuza na kuendeleza mchezo wa ndondi lakini mambo yamebadilika na kujikuta kwenye deni kubwa.

Wakili Patrick J. Neligan amesema Mei 25, 2015 kampuni hiyo ilitangzwa rasmi kwamba imefilisika na itakuwa chini ya mahakama mpaka hapo itapofanikiwa kurudisha madeni ya watu na kuwa sawa kujiendesha yenyewe.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging