Google PlusRSS FeedEmail

MAINA NA MWINYIMKUU WAFUNGA NDOAWANAMUZIKI wa taarabu Maina Thadei na Mwinyimkuu a.k.a Silver Stone wametangaza rasmi kwamba wapo ndani ya ndoa.

Wawili hao toka bendi moja ya Le Grande Utalii, wamefunguka na kuweka wazi kwamba kabla ya ndoa hiyo walikuwa wapenzi kwa muda wa miaka minne.

Walitangaza hilo jana mchana kupitia kipindi cha Mitikisiko ya pwani kinachorushwa kituo cha timesfm.Mwinyimkuu alisema kwamba” Haikuwa rahisi kwa Maina kukubali kwamba ningemuoa, na ilikuwa suprise kwake kwani nilimwambia nataka kumuoa asubuhi moja tulipoamka, na alishangaa sana”

Naye Maina alisema “ni kweli tumefunga ndoa na tunamuomba Mungu atusaidie kwani tumekaa kwa muda mrefu na tayari tumeshaelewana”

Bi Hindu na Dida walitumia kipengele cha Kungwi kwenye kipindi cha Mitikisiko ya Pwani, kuwatakia heri wawili hao huku wakiwaasa wakae kwa amani na upendo.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging