Google PlusRSS FeedEmail

RITA AIPA KISOGO SIASAMwanamama anayeongoza kwa kuwavutia vijana wengi wa kike hapa nchini waweze kujiamini kwa kile wakifanyacho , Rita Paulsen maarufu kama “Madam Rita” amefunguka na kusema kwamba hana mpango na hafikirii kuwa Mwanasiasa.

“Nina mambo mengi ya kufanya yanayoweza kunisaidia kufika mbali na kufanikiwa kwenye maisha yangu ila sio siasa” alijibu Madam Rita pale alipoulizwa swali na mwandishi wa timesfm.co.tz kuhusu mpango wa kuwa mwanasiasa hapo baadae.

Madam Rita alizidi kufunguka kwa kusema kwamba yeye sio muongeaji sana, na siasa inahitaji mtu muongeaji, lakini aliweka tahadhari kwamba hajui mwisho wake hivyo lolote huweza kutokea.

Pamoja na hayo Madam aliwasisitiza watanzania kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kwa ajili ya kupiga kura kwenye uchaguzi mkuu wa oktoba ilikuwachagua viongozi wanaowaona wanafaa kuliongoza Taifa la Tanzania.

Kuhusu kipindi chake cha Bongo Star Search, Rita amesema shindano hilo lipo na litafanyika ndani ya mwaka huu, huku akiwataarifu watanzania wakae tayari pia kupokea kipindi chake kipya cha tv ambacho kitaanza hivi karibuni.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging