Google PlusRSS FeedEmail

WASHINDI WA BSS WANALIPWA PESA TASILIMUChief judge na mkurugenzi wa kampuni ya Benchmark production inayoandaa shindano la muziki la Bongo star search “Ritha Paulsen” amesema uvumi unaoenea mitaani kwamba huwa hawalipi pesa washindi wa shindano hilo ni wakupuuzwa.

Akifunguka jijini Dar es Salaam Madame amesema taarifa hizo zinalengo la kuwachafua na kwamba kama kweli wangekuwa hawalipi basi BASATA ingewafungia.

“Shindano la bongo star search ni mwaka wa nane tunafanya, nafikiri tungekuwa tushafungiwa kawaida zawadi hizo tunaziwakilisha kwa BASATA, waulizwe hata hao wanaochukua watakwambia si kweli” alisema Ritha.

Katika line nyingine Madame amefunguka kuwa, shindano hilo litafanyika kama kawaida mwaka huu na kipindi kipya ambacho kitaitwa Ritha Paulsen show.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging