Google PlusRSS FeedEmail

WEMA SEPETU ACHOKA KUTUKWANA

Makundi na watu mbalimbali wamekuwa na mijadala mizito katika kuichambua, sheria mpya ya makosa ya kimtandao ambayo ilitungwa na bunge la jamuhuri ya muungano wa Tanzania.

Chama cha wamiliki wa tovuti nchini, imefanya vikao mara kadhaa na kutoa waraka wakimsihi Rais Kikwete kuto Kuisaini sheria hii kwa sababu itapelekea watumiaji wa mitandao kutokuwa na uhuru wa kuzungumza na kutoa maoni.

Wema Sepetu ni mmoja kati ya wahanga ambao wamekumbana na mikasa ya “Cybercrime” au “Cyberbulling” mitandaoni, kwa mara ya kwanza ameonesha hisia zake za wazi katika kuikubali sheria hii kwa kile anachokiona itamlinda dhidi ya kadhia anayoipata mara kwa mara kwenye mitandao.

Star huyo wa bongo movie ametoa mtazamo wake kupitia kwenye ukurasa wake wa Instagram, akidai amechoshwa na vitendo vya kidhalilishaji anavyofanyiwa na hata muda mwingine watu wamekuwa wakimshambulia kwa matusi ya nguoni mama yake mzazi.

“Ukweli ni kwamba watanzania tunatumia vibaya mitandao ya kijamii, matusi yamekuwa mengina sometimes hawavumiliki .kwa kweli kuna hitaji kuwa Law na place za kupunguza unyanyasaji katika mitandao ya kijamii.that said yes naisapoti hii bill ya Cybercrime to an extend” aliandika Wema

Katika line nyingine Wema amewatupia lawama wanasiasa, kuwa wametunga pia sheria hii ili kuwaziba watu midomo. Madame amedai amechoshwa kutukanwa na kudhalilishwa kila siku, huku wengine wakienda mbali zaidi kwa kumporomoshea mama yake matusi ya nguoni.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging