Google PlusRSS FeedEmail

ALLY KIBA & JACGUELINE MENGI WAUNGANA NA WILD AID KUPAMBANA NA UJANGILI

          

Msanii wa Bongo Fleva Ali Kiba, Jacqueline Mengi , wameamua kuungana na shiriki la kimataifa liitwalo WildAid ili kupiga vita ya ujangili na biashara ya pembe za ndovu.

Uzinduzi wa kampeni hiyo ulifanyika katika hoteli ya Sea Cliff na kuhudhuliwa na waziri wa Maliasili na Utali, Lazaro Nyalandu na wakiwemo mabarozi wa China na Marekani.

Akizungumza na waandishi wa habari Ali Kiba alisema ‘Nashukuru kwanza nilipata nafasi ya kuishi na tembo porini kwa muda wa siku wa tatu kwa hiyo kiukweli lazima uogope maana mimi ni muoga nambari moja, ila nilichokuwa nafikiria ni tofauti na vile nilivyodhani ila tembo ni wanyama wazuri


Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyarandu akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na uzinduzi wa kampeni mpya ya kupambana na ujangilli wa Tembo uliofanyika katika hoteli ya Sea Cliff jijini Dar es Salaam Juni 18, 2015. Picha zote na CATHBERT KAJUNA WA KAJUNASON BLOG.

Balozi wa Mpya wa Kampeni ya Kupambana na Ujangili wa Tembo, Msanii wa mziki wa kizazi kipya Ali kiba akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na uzinduzi wa kampeni mpya ya kupambana na ujangilli wa Tembo uliofanyika katika hoteli ya Sea Cliff jijini Dar es Salaam Juni 18, 2015.

Afisa Mtendaji Mkuu wa African Wildlife Foundation, Dk. Patrick Bergin akizungumza katika mkutano wa uzinduzi wa kampeni ya sifa ya wanyamapori katika hotel ya Sea Cliff jijini Dar es Salaam Juni 18, 2015.

Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhaji Mussa Salum akizungumza na waandishi wa habari leo katika hoteli ya Sea Cliff jijini Dar es Salaam Juni 18, 2015.

Balozi wa Mpya wa Kampeni ya Kupambana na Ujangili wa Tembo, Msanii Jacqueline Mengi kuhusiana na uzinduzi wa kampeni mpya ya kupambana na ujangilli wa Tembo uliofanyika katika hoteli ya Sea Cliff jijini Dar es Salaam Juni 18, 2015.

Balozi wa Mpya wa Kampeni ya Kupambana na Ujangili wa Tembo, Msanii wa mziki wa kizazi kipya Ali kiba akizungumza na waandishi wa habari.
Viongozi wa Dini waliofika katika uzinduzi huo wakifuatilia kwa makini...

Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyarandu akizungumza na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhaji Mussa Salum.


Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyarandu akiwa katika picha ya pamoja na Mabalozi wa kampeni hiyo.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging