Google PlusRSS FeedEmail

BAADA YA KUPOKEA HABARI MBAYA ESHA APIMA UKIMWI

MSANII wa filamu, Esha Buheti ajikuta katika wakati mgumu mara baada ya kupokea habari mbaya zilizompelekea kwenda kupima UKIMWI.

Amebainisha hayo leo kupitia ukurasa wake wa nstagram baada ya kutuma majibu ya vipimo alivyochukua baada ya kupima ugonjwa wa UKIMWI.

Esha ametumia “time” yake kuihasa jamii, kuhamasika kupima virusi vya UKIMWI akiwataka kuto ogopa kwa maana kila jibu litakalotoka kuna namna ya kuweza kuishi kwa kufata taratibu ulizo pangiwa na wataalam.

Mwigizaji huyo amepost fomu ya majibu iliyodhihirisha hana virusi vya ukimwi(negative), na caption ambayo imefafanuliwa na wazee wa ubuyu kuwa mwenzi wake “alichepuka” na baada ya Esha kupewa taarifa ndipo alipoamua kwenda kupima.

“Kupima sio Kazi Kazi Ni kuchukua majibu…., y tumekua waoga sana kupima? Nahisi Ni vzr kuijua afya yako….. Haimaanishi kama ukikutwa na HIV Ndo mwisho wa maisha yako kwa upande Wangu mm hakuna ugonjwa nauogopa kama cancer…… Jana nlipoenda kupima nlikutana na mwandishi wa habari na nikamwambia nipo tayari kwa jibu lolote alinihoji y nimekua jasiri sana! Kiukweli kupokea majibu kunahitaji ujasiri….. Na nlimwambia kama ntakua ninao naomba niwe msanii wa kwanza kujitangaza……. Kuna habari mbaya sana nlizipokea ikanibidi niende kupima majibu yalipotoka sikuamini wallah mungu ananipigania sana Nasitaacha kumtumia…. Ushaurii tuuu Ni vizuri kujua afya zetu coz hakuna anaejua nyendo za mwenzi wake…… Team amasisha#wengine# Tanzania bila ukimwi inawezekana” ameandika Esha.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging