Google PlusRSS FeedEmail

BECKA TITLE KUOA HIVI KARIBUNI

HATIMAYE Mkali wa chorus toka kundi la muziki B.O.B, Becka Title amevunja ukimya na kuweka wazi kuwa mwanamke atakayemuoa ni yule aliyezaa naye mtoto wa kwanza.

Beka ambaye miaka miwili ya hivi karibuni ameonekana kufanya vizuri kwenye game ya Bongo Flava, huku akipata collabo nyingi toka kwa wasanii wachanga na wakongwe, amesema amefurahi kupata mtoto wake wa kwanza na anampenda sana girl friend wake.

” Kwanza namshukuru Mungu kwa kupata mtoto, kitu ambacho nilikuwa nakifikiria na kusubiri kwa muda mrefu, sasa hivi nina mtoto anaitwa Allyah, na Mungu akipenda basi nitamuoa Mama Mtoto wangu “, alisema Becka.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging