Google PlusRSS FeedEmail

G NAKO HAIMSUMBUI KUKOSEKANA KWENYE TUZO ZA KILIMANJARO

Mkali wa chorus za hipohop za muziki wa bongo, G Warawara a/k/a G Nako toka kundi na kampuni ya Weusi amefunguka na kusema kwamba hajisikii vibaya yeye kutokuwepo kwenye kipengele chochote cha tuzo za Muziki za Kilimanjaro mwaka huu, huku wenzake Joh Makini na Nikki wa pili wakiwemo kwenye tuzo hizo.

“Mbona mimi nilitajwa mwaka jana, kwa mwaka huu kutotajwa kwangu haimanishi kwamba mimi sio mkali au wao ni wakali zaidi yangu, ni bahati na utaratibu tu, lakini hakuna tatizo kwani Joh na Nikki wa pili wanawakilsha Weusi basi wataniwakilisha”, alijibu G Nako alipoulizwa swali je anasemaje kuhusu yeye kutokuwepo kwenye tuzo za kill wakati wenzake anaofanya nao kazi pamoja wametajwa kushiriki kwenye tuzo.

G Nako alizungumzia pia tamko lake la kupunguza kufanya collabo, na kusema kwamba amefikia kiwango alichojipangia kufanya collabo kwa hiyo atapunguza collabo na kushirikishwa kwa muda ili ajipange zaidi kufanya kazi zake.

Kundi la Weusi limekuwa likifanya vizuri kwa miaka ya hivi karibuni kwenye muziki wa hiphop wa hapa nyumbani na mwaka kundi hilo linawania moja ya tuzo za muziki za kilimanjaro, pamoja na Wanamuziki Joh Makini, Nikki wa pili ambao pia wanatoka ndani ya kundi hilo.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging