Google PlusRSS FeedEmail

JAY Z AKUMBWA NA SHTUMA ZA UBAGUZI WA RANGITukio la kuuwawa kwa kijana mwenye rangi nyeusi na askari wa mji wa Baltimore huko Marekani limeleta sura mpya kwa waamerika weusi na kuona kwamba wanabaguliwa.

Watu wengi mashuhuri wakiwemo wanamuziki kama Jay Z walionekana kukwerwa na tukio hilo ambapo licha kutumia vyombo vya habari televishen na radio pia alitumia mitandao yake ya kijamii kupinga tukio hilo.

Lakini licha ya kukwerwa na tukio hilo, Ijumaa ya wiki hii Jay Z na mkewe Beyonce walijikuta matatani na kuishia kusemwa kwa maneno makali kutoka kwa mashabiki na wadau wa muziki na waamerika weusi waliotumia akaunti zao za mitandao ya kijamii kuwasema kwa maneno makali Jay Z na Beyonce mara baada ya wapendanao hao kuonekana wakiwa kwenye picha ya pamoja na wazungu watupu.

Picha hiyo iliwaonyesha Jay Z na Beyince wakiwa nchini Norway walipokuwa wamekwenda kufungua ofisi ya program mpya ya Jay Z inayojulikana kwa jina la Tidal Music itakayowasaidia Wanamuziki kupata fedha.

Wengi walihoji kwa nini ofisi ya chini Norway iwe imejaa wazungu peke yao je inamaana hakuna watu weusi?

Mmoja wa mashabiki aliandika ” asilimia 97 ya wafanyakazi wa ofisi ya tidal huko Norway ni wazungu, haiwezekani”.

Wapo waliojaribu kuwatetea wawili hao, na kusema kwamba ofisi iliyopo Rorway ni nchi ya ulaya hivyo wazungu ni lazima wawe wengi, lakini watu hawakusimama kushusha madongo.

” Jay Z aliwahi kutulaumu watu weusi, kwamba watu weusi hawawezi kusaidiana wenyewe kwa wenyewe, sasa yeye ndio anafanya nini”, aliandika mdau mmoja kwenye akaunt ya twitter.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging