Google PlusRSS FeedEmail

KENDRICK AFANYA SURPRISE KWA MASHABIKI WAKERapa anayezidi kujipatia umaarufu kila kukicha kwenye game ya muziku huko nchini Marekani, Kendrick Lamar, jumatano ya wiki hii aliwafanyia surprise madent wa shule ya ufundi North Bergen huko New Jersey nchini Marekani baada ya kuingia darasani na kushiriki katika mada ya uchambuzi wa mashairi.

Mada hiyo iliyokua ikiongozwa na kufundishwa na Mwalimu wa somo la kingereza, Brian Mooney ambaye hakuwataarifu Wanafunzi wake kabla kama kutakuwa na mgeni ambaye ni Kendrick Lamar ambapo siku hiyo walikua wanachambua kitabu cha mashairi “The Bluest Eye” kilichotungwa na Toni Morrison.

Baada ya uchambuzi huo, Kendrick Lamar alitoa nafasi kwa wanafunzi hao kuonyeshana ujuzi wa kuchana mitindo huru, (Freestyle).

Kendrick Lamar, alisema “Mara nyingi ninapowasikiliza wanafunzi huwa napata kitu kipya, muda wa kuwasikiliza ndipo ninapoweza kuwafahamu uwezo wao, ni vizuri na nipo kwa ajili ya kuwasaidia ili wafikie mbali kisanaa”.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging