Google PlusRSS FeedEmail

LIL OMMY AACHIA 'MAGAZINE' YA THE PLAYLIST YENYE STORY ZA MASTAA WA BONGO


MTANGAZAJI wa kipindi cha The Playlist cha 100.5 Times Fm, Lil Ommy (Omary Tambwe) ameamua kutoa jarida maalum la ‘The Playlist’ litakalobeba maadhuhi ya kipindi chake ili  kuhakikisha wasikilizaji wa kipindi hicho wanafikiwa na burudani iliyoambatana na elimu itakayobebwa kwenye jarida hilo, ambalo litapatikana bure katika Malls mbalimbali ikiwemo, Mlimani City, Msasani Mall na Maduka Makubwa Bongo.

Jarida hilo pia litatoa nafasi kwa baadhi ya wasikilizaji waliopitwa na mastory ya kipindi hicho cha ‘The Playlist’ kuweza kusoma yaliyojiri ndani ya kipindi hicho, kupitia jarida hilo litakalokuwa linatoka kila baada ya mwezi.

Katika jarida hilo, wakali wa Bongo Fleva kama Diamond Platinumz, Vanessa Mdee, Ommy Dimpoz na Jokate Kidoti wamefunguka bila kuacha nukta mengi ambayo fans wao wangependa kuyafahamu kuhusu maisha yao ya muziki.

Pia kuna special coverage ya burudani nje ya muziki ikiwemo series iliyoiteka dunia ya burudani ya filamu kutoka Marekani, Empire.

Jarida la THE PLAYLIST lipo kitaani hivi sasa katika Malls kama vile Mlimani City, Msasani Mall na Maduka Makubwa Bongo, kufahamu zaidi jinsi ya kulipata bure, sikiliza 100.5 Times Fm.

kwa mujibu wa Lil Ommy, THE PLAYLIST Magazine litakuwa likitoka kila baada ya miezi na kushirikisha Mastori ya wasanii wote walikuja kwenye kipindi chake kwa muda huo.

Usikose kusikiliza The Playlist kila Jumapili saa kumi hadi kumi na mbili jioni ambapo Star au Mtu Maarufu anadondoka ndani ya Studio kuchagua ngoma tano kali anazopenda na kupiga interview ya kibabe na wasikilizaji wanapata nafasi ya kuuliza maswali yao kupitia SMS na Mitandao ya kijamii. #thePLAYlistMcheki Lil Ommy kwenye Twitter na Instagram kwa info zaidi @LilOmmy

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging