Google PlusRSS FeedEmail

MATUNZO YA MTOTO YAMPELEKA SELO DMX

Rapa aliyewahi kuvuma kipindi cha miaka ya nyuma Earl Simmons a/k/a DMX ijumaa ya june 26 mwaka huu alikamatwa na polisi na kutupwa selo kwa kosa la kushindwa kutoa matumizi kwa moja ya mtoto wake.

Kabla ya kukamatwa kwake, siku hiyo rapa huyo alikuwa na ratiba ya kufanya show ya radio Nw York City na wakali wenzake wa enzi hizo Rakim, Ma$e, The Lox na Pete Rock.

DMX, (44) Baba wa watoto 12 hii sio mara ya kwanza kutupwa selo kutokana na kushindwa kulipa fedha ya matumizi kwa watoto kwani hata mwaka 2006 aliwahi kukamatwa kwa kufanya kosa kama hilo.

DMX, amekuwa na matukio ambayo sio mazuri kitendo ambacho kinamfanya afikishwe mahakamani na gerezani mara kwa mara.

Uuzaji wa madawa ya kulevya, kukaba na kupigana imekuwa ni jambo la kawaida kwa mkongwe huyo.

Kumpiga Manny Pacquiao pekee haikua sababu kuu ya Floyd Joy Mayweather kupata tuzo ya Mwanamichezo Bora wa mwaka kwa Wanaume, kwenye Tuzo za BET mwaka huu. Ingia kwenye website ya timesfm.co.tz au bonyeza hiyo link hapo kwenye Bio yetu uckeck list nzima ya washindi wa tuzo za BET.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging