Google PlusRSS FeedEmail

MKOLONI NA SIASAMwanamuziki Mkongwe kwenye game ya Bongoflava Fred Mariki a/k/a Mkoloni toka kundi la Wagosi Wakaya amerudi tena na safari hii anaachia ngoma yake mpya inayoitwa Tupo Pamoja.

Wakati akipiga stori na Mwandishi wa timesfm.co.tz Mkoloni alisema, anaachia wimbo huo sababu ni kipindi muafaka ambapo Nchi inaelekea kwenye mchakato wa Uchaguzi Mkuu kulingana na ujumbe uliopo ndani ya wimbo huo.

“Kama Wagosi Wakaya, kila siku tumekuwa tukiigusa jamii inayotuzunguuka, na safari hii pamoja nakuwa wimbo wa tupo pamoja nimeimba kama solo artist lakini siwezi kutoka kwenye misingi ya Wagosi Wakaya, hivyo naomba jamii iupokee wimbo huu kwani ni kwajili ya elimu tosha juu ya maisha yao ya kila siku, kabla ya uchaguzi na baada ya hapo uchaguzi utakapokwisha”, alisema Mkoloni.

Kuhusu, kundi la wagosi Wakaya, Mkoloni amesema kundi lipo kama kawaida na baada ya kutoa nyimbo mbili zilizopita (Ghawana na Bao), wanajiandaa kuachia albamu yao ya pamoja iitwayo Muamsho ambayo tayari imekamilika na muda wowote mwaka huu wataipata mitaani kwao.

Mkoloni alimalizia kwa kusema wimbo wa Tupo Pamoja umetengenezwa kwa ushirikiano wa maproducer wawili, Jors Bless wa Sababisha Records na Hammy B wa BHits na utatoka rasmi jumatatu ijayo ya tarehe 1 mwezi June.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging