Google PlusRSS FeedEmail

MRISHO MPOTO AKANUSHA KUTUMIKA KISIASAMkali wa muziki wa kughani (mashairi) nchini Mrisho Mpoto, amezungumzia tuhuma zinazoelekezwa kwake kuhusu kutumika kisiasa na kulaghai jamii, amedai si za kweli na zina lengo la kumchafua.

Akifunguka kupitia kipindi cha “the jump off” cha Times fm, Mpoto amedai shughuli nyingi anazozifanya kiserikali ni za kuhamasisha jamii katika maswala ya Elimu, Afya na maendeleo zaidi.

“Unajua mi nashindwa kuelewa, kwa mfano nikienda Kigoma kuhamasisha wananchi juu ya maswala ya kutumia Chandarua kuepuka malaria kuna tatizo gani? nikihamasisha watu wajiunge na bima za Elimu kunatatizo gani?, mimi situmiki eti kuwafunga midomo wananchi hapana, wala situmiki kisiasa nafanya vitu kwa maendeleo ya jamii ni watu tu wanaona kama natumika na chama Fulani eti” alisema Mrisho

Katika line nyingine mjomba amewaasa wasanii, kuwa makini katika kampeni za kisiasa wanazoalikwa kuelekea uchaguzi mkuu, waungane na viongozi wanaokubalika na wananchi

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging