Google PlusRSS FeedEmail

MTOTO AMPONZA P. DIDDY

JUMATATU  ya jana Mwanamuziki ambaye pia ni  mjasiriamali Sean John Combs a/k/a P Diddy alikiona cha moto baada ya kutupwa jela ya Chuo Kikuu cha California kwa muda kabla hajaachiliwa kwa dhamana.

Mapema siku ya jana Mwanamuziki huyo alifika maeneo ya chuo hicho na kwenda kumuangalia mtoto wake Justin Combs wakati afanya mazoezi ya mpira.

Wakati Mtoto Justin akiendelea na mazoezi pamoja na wenzake ghafla walirumbana na kocha wa timu yao, Sal Alosi, kitendo ambacho kilimfanya Mwanamuziki huyo kuingilia kati na kusababisha zogo kwenye eneo hilo.

Baada ya zogo hilo Kocha Mkuu wa timu ya Chuo hicho ndugu Jim Mora aliita polisi ambao walimtia nguvuni P Diddy na kwenda kumtupa rumande na baada ya mazungumzo kwa muda, Diddy aliachiliwa kwa dhamana ya dola elfu 50,000 huku kesi ikipangwa kusikilizwa tena July 13 mwaka huu.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging