Google PlusRSS FeedEmail

MWASITI AJITANGAZA KUWA MBABE

Serebuka ni ngoma inayoendelea kufanya vizuri kwenye vyombo mbalimbali vya habari hapa nchini. Ngoma hiyo ambayo inaonekana kugusa watu wengi kutokana na ujumbe uliomo ndani yake ambao unahamasisha watu kuendelea kuwa na furaha pamoja na kutendwa katika maisha yao ya mahusiano.

Staa aliyeimba wimbo huo Mwanadada, Mwasiti amejibu tuhuma za wale wote wanaodhania kwamba amepotezwa na wasanii wapya wa kike walioibuka kwenye game ya Bongo Flava.

“Kila mmoja ana ladha yake, na kila mmoja ananafasi yake, mimi nipo na nitaendelea kuwepo na hakuna anayenitisha”, Amefunguka Mwasiti,

Kuhusu kukaa muda mrefu kwa yeye baada ya kutoa ngoma moja, Mwasiti amesema huo ndio utaratibu wake kwani tangu 2009 enzi za wimbo wake wa Nalivua Pendo mpaka leo kila mwaka amekua na utaratibu wa kutoa single moja moja.

Mwasiti, hakusita kuwapa pongezi wanamuziki wapya wa kike walioibuka na kufanya vizuri huku akiwatahadharisha kuwa makini kwenye kazi zao.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging