Google PlusRSS FeedEmail

PDM MOVIE KUACHIA AHSANTE RAMADHANI YA MSHINDO

              Ahsante Ramadhani Films

KAMPUNI ya PDM Movie katika kuukaribisha mwezi mtukufu wa Ramadhani inaachia filamu kali nay a kusisimua ya AHSANTE RAMADHANI kutoka kwa mwigizaji na mwongozaji mahiri katika tasnia ya filamu Bongo Mshindo aka J- Four.

Mshindo Jumanne muongozaji na mwigizaji wa filamu Bongo anakuja na filamu maalum kwa ajili ya mwezi Mtukufu wa Ramadhani inayoitwa Ahsante Ramadhani kwa ajili ya waumini wa kiislamu kama zawadi kwa wapenzi wa filamu kwa mara ya kwanza itasambazwa na PDM Movie.

“Nimeamua kutengeneza filamu ya Ahsante Ramadhani kama zawadi kwa wapenzi wa filamu, kila siku natengeneza sinema za kawaida sasa naona muhimu sana kumkumbuka Mola kwa njia ya filamu,”anasema Mshindo.

Mshindo amedai kuwa anaona fahari kwa kuwakumbusha Waislamu kuongelea neno la Mungu kwani sinema za aina hiyo ni chache sana tofauti na sinema za mapenzi na mambo mengine filamu hiyo inasambazwa na PDM Movie au Saiprima wakati sinema nyingi Mshindo usambaza mwenyewe.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging