Google PlusRSS FeedEmail

PROFESSA JAY "NIKIINGIA BUNGENI NITAHAKIKISHA UMOJA WA WASANII"MSANII mkongwe wa muziki wa kizazi kipya nchini Joseph Haule Profesa Jay, amebainisha kuwa kuunda umoja na kuhakikisha maslahi ya wasanii yanasimami ipasavyo ndio jambo la kwanza atakaloakikisha analifanya pindi akipata ushindi wa kuingia katika bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

Aliyazungumza hayo mara baada ya kushinda tuzo ya KTMA, Wimbo bora wa Hip Hop ambapo aliweka wazi kuwa moja ya mkakati wake pindi akichaguliwa ubunge ni kuhakikisha wasanii wanakuwa wamoja ili waweze kutetea maslahi yao kwa pamoja.

Professa Jay alishatangaza nia ya kugombania ubunge katika jimbo la Mikumi mjini Morogoro, huyu hatokuwa msanii wa kwanza kuingia bungeni kwani teyari Sugu ni miongoni wa wasanii ambao wameingia bungeni kwa kupitia tiketi ya chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA.

Alisema kuwa atapambania kuhakikisha wasanii wanakuwa na umoja wao ili kuweza kuhakikisha unakabiliana na changamoto zao kwa kuzipanga kwa kipaumbele.

“Unajua kila msanii analia na changamoto hizi wapo wanaodai soko bovu wengine wanalia na mapromota huku wapo wasanii wanaolia na serikali kushindwa kuziba mianya ya wizi katika kazi za sanaa” alisema Jay.

Alisema kuwa inapaswa wasanii wote kuwa na kauli moja ili kuweza kupambana na changamoto hizo wanazokabiliana nazo.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging