Google PlusRSS FeedEmail

RAPA IGGY AZALEA 'AMVAA NICK" MINAJ

Ni wiki kadhaa zimepita tangu Nick Minaj atupie picha zilizoonyesha kuwa amevalishwa pete na boyfriend wake Meek Mill, sasa mkali mwingine wa rap kwa upande wa Wanawake kutoka nchini Marekani Iggy Azalea ameshare picha zake kwenye mtandao wa Instagram, akionyesha kuwa amevalishwa pete ya uchumba na mpenzi wake ambaye ni mchezaji wa mpira wa Kikapu ( Basketball) .

Iggy ambaye anaonekana kuwa mpinzani wa Nick Minaj kwenye tasnia ya rap, inaripotiwa kuwa alivalishwa pete hiyo na mpenzi wake Nick Young, jumatatu ya tarehe 1 june siku ambayo ilikuwa ni siku ya kuzaliwa kwa Nick Young.

Sherehe hiyo ilihudhuriwa na watu wachache wa karibu wa wapenzi hao, ambapo baada ya Nick Young kumvalisha pete Iggy wote wawili walikubaliana na kuahidi mbele ya wageni waalikwa kwamba wataoana.

Baada ya tukio hilo Iggy alitupia picha ya mkono wake ukiwa na pete ya uchumba huku ikiwa na caption…..Happiest Day#Isaidye……..

Nick Young ametimiza miaka 30 na Iggy ana miaka 25 huku ikiripotiwa wawili hao walianza uhusiano tangu mwaka 2013.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging