Google PlusRSS FeedEmail

SERIKALI HAMUONI FAIDA ZA WASANII NCHINI??

“Mziki wetu umekuwa sana hivi sasa, kila mtu anafanya kwa uwezo wake”, hiyo ni kauli ya Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Slaa akizungumza jijini Dar es Salaam.

Ni dhahiri kwamba “game” yetu imekuwa kwa asilimia kubwa hivi sasa, kwani hata ilipoonekana  post ya Television kubwa Africa “MTV” kwenye Instagram, ikiongelea kuhusu kuachia nyimbo mpya ya Diamond “NANA” aliyomshirikisha MR Flava, haikushtua sana kwa maana ni kitu ambacho tunaelekea kukizoea hivi sasa.

Well wakati Plutnumz akifanya hayo, hasimu wake wa karibu “Ally kiba” ameshare picha kadhaa IG zikionyesha muda mwingi anautumia studio “Combination sound” kwa ajili ya kutuletea ngoma inayofuata baada ya Chekecha.

“Mzigo mwingine huo baada ya #chekecha #cheketuavideo #kingkiba” ameandika kupitia Instagram.

Hii ni ishara nzuri kwamba tunaendelea vizuri na tasnia hii, ambayo imeajiri vijana kwa asilimia kubwa nchini kwetu.

Swali? Unafikiri serikali imeweka mkazo katika kusimamia maslahi ya wasanii??

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging