Google PlusRSS FeedEmail

THE GAME CHUPUCHUPU KUTUPWA JELARapa the Game, huenda juma hili lingehitimisha maisha yake gerezani baada ya kumtwanga mtu ngumi wakati wakicheza mpira wa basketball.

Tukio hilo lilitokea mwishoni mwa mwezi march mwaka huu, na kesi hiyo ilikua ikiendelea kimyakiya kabala ya The Game jumatatu ya june 8 kuamua kulipa faini ya dola za kimarekani elfu 50.

Siku ya jumatatu alionekana The Game akiingia kituo cha polisi na kwenda kulipa faini na baada ya dk 54 The Game aliachiliwa huru.

Kipande cha video kutoka mtandao wa TMZ kinaonyesha The Game akimpiga mtu ngumi wakiwa katikati ya mchezo. Katika ripoti yake aliyoiandika polisi The Game aliamua kumpiga ngumi kijana huyo kwa sababu mara ya kwanza wakati wapo kwenye mchezo alisukumwa na kijana huyo.

Kwa mujibu wa polisi, kosa la The Game ni pale alipotampa kwamba atamuua kijana huyo wakati akimalizia kumpiga ngumi.

Baada ya kumalizana na kesi hiyo, kupitia akaunt yake ya instagram The game alipost picha akiwa amepozi kwenye swimming pool na kuiweka caption yenye maneno haya ”Relaxing in the sauna before I turn myself in But what you gone do when you get outta jail… I’m gonna have some fun”.

Bofya hii link hapa chini, uone kipande cha video kinachomuonyesha The Game akimtwanga ngumi mwenzake

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging