Google PlusRSS FeedEmail

UMEISIKIA HII RAPA WA LIL WAYNE ASAKWA KWA MAUAJI

Kwa mujibu wa mtandao wa habari New Orleans Times-Picayune, Polisi wa mji wa Eastern New Orleans wamethibitisha kumuona rapa Widner a/k/a Flow kuhusika kwenye tukio la mauaji la ndugu wawili Kenard na Kendrick Bishop, lililotokea may 25 mwaka huu.

Mili ya ndugu hao ilikutwa kwenye gari, vipande vya video kutoka kwenye kamera za usalama zilizotegeshwa katika eneo lililotokea mauaji vilimuonyesha Flow akitoka kwenye gari hilo pamoja na mwenzake ambaye hakuweza kufahamika.

Tayari polisi wametoa tangazo la kumsaka na kumkmata rapa huyo, huku wakiomba wanachi wenye taarifa zaidi kuhusu mauaji hayo wazitoe haraka ili uchunguzi uendelee kufanyika.

Rapa Flow alisaini mkataba na kampuni ya Lil Wayne “Young Money Entertainment” mwaka 2012 na habari zinaeleza kwamba sauti yake itasikika kwenye mixtape mpya ya Lil Wayne inayotarajiwa kutoka hivi karibuni.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging