Google PlusRSS FeedEmail

YEMI ALADE ASHUSHA MAZITO KWA WAANDAAJI WA TUZO ZA BET

                                  

Baada ya msanii Fuse ODG, kusema sababu za yeye kutohudhuria kwenye kilele cha Tuzo za BET kilichofanyika usiku wa june 28, siku ya Jumapili kwamba ni kwa sababu wasanii kutoka Afrika wanapewa tuzo hizo Backstage (Nyuma ya Jukwaa).

“Kwa nini wasanii wa Afrika wapewe Tuzo hizo nyuma ya jukwaa?”, alihoji Fuse ODG mwanamuziki kutoka nchini Ghana hivyo hakuona maana ya kuhudhuria pamoja na kwamba alitajwa kwenye kuwania tuzo hizo.

Pia Msanii WizKid wa Nigeria alisema naye hakwenda kwenye Tuzo hizo kwa sababu aliona Waafriaka wanadharaulika.

Kwa kutumia akaunti yake ya instagram, Mwanamuziki Yemi Alade kutoka nchini Nigeria naye ameonyesha kukerwa na kitendo hicho ambacho amekiita ni udhalilishaji kwa wasanii na Bara la Afrika.

Yemi Alade aliandika maneno yenye maana ya kuhoji, Kwa nini wasanii wa Afrika wanadharauliwa kwa kupewa tuzo hizo saa nne kabla ya tuzo zenyewe kufanyika?.

Yemi aliwataka wasanii wenzake wa Afrika kuungana kufikisha ujumbe huu kwenda kwa waandaaji wa BET, isijirudie tena au kama haiwezekani ni bora Waafrika wasitajwe kabisa.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging