Google PlusRSS FeedEmail

2 CHAINS KUSHTAKIWA TENA KWA UDHALILISHAJI



Mwezi wa sita Mwanzoni, tulikujuza kuhusiana na binti wa kimarekani anayetaka kumshtaki rapper wa Atlanta 2 Chains, kwa kosa la kusambaza video ya kudhalilisha dhidi yake.

Akizungumza na kituo cha Television cha WBTV, msichana huyo ‘Christine Chisholm’ amesema alifungua kesi mwanzoni na anashangaa mwanasheria wa 2chains kutotilia maanani.

“Mimi waliniita back stage, sikujua kama wananirekodi walikuwa wananigeuza geuza huku akicheka na wenzake, baada ya siku kadhaa naiyona Youtube mpaka kazi nikafukuzwa na kila sehemu ninayopita naonyeshewa vidole” alisema Chisholm.

Binti huyo aliongeza kuwa, safari hii amejipanga vilivyo na anahitaji alipwe mkwanja wa dola za kimarekani milioni 5.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging