Google PlusRSS FeedEmail

LINAH APATA DILI LA KUSOMA

MUIMBAJI wa muziki wa kizazi kipya nchini Linah Sanga 'Linah' amepata donge nono la kwenda kusoma jinis ya kupiga ngoma 'Drums' hii itampa utofauti mkubwa kati yake na wasanii baadhi wa kike ambao hawana ujuzi huo.

Alianza kuzivujisha taarifa hizi kupitia ukurasa wake wa Instagram, akidai amepata ‘sponsorship’ ya kwenda kusomea upigaji wa ngoma na ala zingine za muziki South Africa.

Akizungumza jijini Dar es Salaam,  Linah, amefunguka na kusema kuwa ‘deal’ hii ameipata muda mrefu kidogo kutoka kwa wadau wa muziki nchini humo.

“Nilienda South Africa kitambo, so tulikuwa tunapiga story tu ndo likagusiwa hili swala la sisi wanawake kuogopa kujaribu vitu vingine, mi nikawaambia natamani kusomea basi ikaishia hapo

sasa juzi nmeenda kule wakakumbushia na kunipeleka chuoni hapo, wakasema wapo tayari kunilipia miezi 7″ Alisema Lina.

Kwenye ‘line’ nyingine, mrembo huyo amedai anasubiriwa yeye tu atoe jibu la ni lini atakuwa tayari kuanza rasmi mafunzo hayo.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging