Google PlusRSS FeedEmail

MUZIKI KUORODHESHWA KWA UMRI UINGEREZAMiziki inayowekwa kwenye mitandao sasa itaanza kuorodheshwa kulingana na umri wa watu ambao wataruhiwa kutizana sawa na jinsi filamu zinavyoorodheshwa

Makampuni ya muziki ya Sony, Universal na Warner yatatuma video kwenda kwa bodi ya filamu ya Uingereza kabla video hizijawekwa kwenye mitandao ya You Tube na Vevo.

Kati ya video 132 zilizowasilishwa kwa bodi hiyo 56 ziliorodheshwa katika kiwango cha 12 huku 53 zikiorodheshwa kiwango cha 15.

Mfano ya video ambazo zinarodheswa kiwango cha 15 ni pamoja na Open Wide ya Calvin Harris na Meet Me in the Midle ya Jessie Ware.

Viwango hivyo vitatolewa kwa video za muziki ambazo hutolewa nchini Uingereza.

Wasanii wa kimataifa ambao huzua utata kupitia kwa video zao kama Rihanna na video yake ya Better Have My Money hawataathiriwa.

Serikali inasema kuwa mpango huo utawalinda watoto kutokana na kutizama video zisizostahili kupitia kwa mitandao.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging