Google PlusRSS FeedEmail

SUGU " HAKUNA UMOJA WA WASANII"


MSANII wa Muziki wa kizazi kipya nchini Jospeh Mbilinyi ‘Sugu’ ambaye pia alikuwa mbunge wa Mbeya Mjini ameshangazwa na kitendo cha watu wachache kuudanganya umma wa watanzania juu ya mualiko uliotolewa na Umoja wa wasanii kumuaga Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Jakaya Kikwete huku akibainisha kuwa ule haukuwa umoja wa wasanii bali ni ‘magumashi’ ndiyo yalitumika kuunda mualiko huo.

Alifafanua kuwa, ule haukuwa umoja wa wasanii, hali ambayo ilipelekea kuibuka kwa maswali mbalimbali ikiwemo usajili wa umoja huo, viongozi wake ni wakina nani, na umoja huo ulianzishwa lini?.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Sugu alisema kuwa kuna baadhi ya watu wachache wameshazoea kufanya ‘magumashi’ kwa kutumia jina la wasanii ili kujinufaisha wao binafsi hali ambayo inaendeleza kudidimiza sekta ya sanaa nchini.

“Mimi ni miongoni wa wasanii wahasisi, lakini nashanga mimi kama msanii sikualikwa, Professa Jay hakualikwa na Rais Kikwete alikuwepo nashangaa hata rais mwenyewe hakuuliza kwa nini wasanii wengine hawakuwepo” alisema Sugu.

Alibainisha kuwa hata bungeni alishawahi kuwasilisha hoja ya kueleza kuwa kuna baadhi ya watu wanamdanganya rais katika masula ya wasanii ili wajinufaishe wao wenye hali hiyo inazidi kukuwa na kugawa matabaka.

Aliongezea kuwa huwezi kuyapeleka mafanikio ya msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini Diamond Platnum kama sifa ya Rais au sifa ya serikali ya awamu ya nne.

Kwa upande wake Msanii wa filamu nchini Haji Adamu ‘Baba Haji’ alisema kuwa mualiko huo ulikuwa ni mualiko feki, kwani kwa upande wake yeye yupo ndani ya Shirikisho la Filamu lakini hakuona kiongozi yoyote aliyeudhuria usiku huo wa kumuaga Rais Kikwete.

“Mimi nasema kuwa ni mualiko feki, kwani rais wangu wa shirikisho la filamu hakuwepo wala hakutoa hotuba, na siku halikwa, na wala sikujua nani aliyekuwa anaalika watu, hakukua na vitu vinavyoeleweka hivyo haikuwa sawa” alisema Baba Haji.This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging